UHAMIAJI, Tangazo la kuitwa mafunzo Jeshi la uhamiaji February 2025

by admin
0 comments
Tangazo la kuitwa mafunzo Jeshi la uhamiaji February 2025
Image with Link Description of Image

Tangazo la kuitwa mafunzo Jeshi la uhamiaji February 2025. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia Vijana ambao wamechaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kuripoti Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Boma Kichakamiba, Wilaya ya Mkinga – Mkoani Tanga, siku ya Jumamosi tarehe 01 Machi, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana. Atakayeripoti Chuoni baada ya muda uliotajwa hatapokelewa. Kwa walioomba na kuchaguliwa kupitia Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kuripoti Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (Tunguu) siku ya Jumatatu tarehe 24 Februari, 2025 saa 2:00 asubuhi

2. NYARAKA AMBAZO MWANAFUNZI ANATAKIWA KWENDA NAZO CHUONI;

Mwanafunzi anatakiwa kuripoti akiwa na vyeti halisi vya elimu na fani mbalimbali. Mwanafunzi ambaye hatokuwa na nayaraka halisi hatapokelewa chuoni. Vyeti na Nyaraka zinazotakiwa ni kama ifuatavyo:-

  • Cheti cha kuzaliwa,
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba,
  • Vyeti halisi (Original) vya Elimu ya Kidato cha Nne, cha Sita na Shahada,
  • Vyeti vya Ujuzi wa aina mbalimbali (Kwa wale wenye ujuzi).

3. VIFAA NA MAHITAJI AMBAYO MWANAFUNZI ANATAKIWA KWENDA NAYO CHUONI

Fedha kiasi cha Tshs. 50,400/= kwa ajili ya Bima ya Afya kwa asiyekuwa na Kadi ya Bima ya Afya au mwenye Kadi ya Bima ya Afya ambayo inaisha uhai wake kabla ya tarehe 31/12/2025, Fedha kiasi cha Tshs. 25,000/= kwa ajili ya vipimo vya afya, Fedha za kujikimu kwa ajili ya matumizi binafsi, Truck suit (02) rangi nyeusi na dark blue, Raba za michezo jozi (02) rangi yoyote, Nguo nadhifu za kiraia jozi (03), Mashuka (04) rangi ya bluu, Mto wa kulalia (01), Foronya (02) rangi ya bluu, Chandarua (01) rangi ya bluu, Madaftari makubwa (04) 4QRs, Sanduku la chuma (Trunker), Ndoo (02) za plastiki (moja ya lita 10 na moja ya lita 20), Fulana (02) rangi ya dark blue zenye shingo ya duara, Viatu vya mvua (rainboot,) jozi (01), Taulo (01), Kandambili jozi (01) pamoja na Vifaa vya Usafi ikiwemo Jembe (01) na mpini wake, Fyekeo (01), Panga (01) na Rake (01).

Aidha, vifaa tajwa vinapatikana katika Duka la Chuo, hivyo mwanafunzi anaweza kuvinunua kwa ridhaa yake.

4. ANGALIZO:

  • i. Gharama za usafiri kutoka nyumbani kwenda Chuoni zitagharamiwa na mwanafunzi mwenyewe.
  • ii. Waliochaguliwa kujiunga na mafunzo watafanyiwa uchunguzi wa afya kabla ya kuanza mafunzo, na wale wote watakaobainika kuwa na changamoto za kiafya hawataruhusiwa kujiunga na Chuo kwa ajili kuhudhuria mafunzo.

Orodha ya Majina ya walioitwa kwenye mafunzo inapatikana

Imetolewa na; Kamishna Jenerali wa Uhamiaji

06 Februari, 2025

You may also like

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Business Hours

  • Monday
    8:00 AM - 9:00 PM
  • Tuesday
    8:00 AM - 9:00 PM
  • Wednessday
    8:00 AM - 9:00 PM
  • Thursday
    8:00 AM - 9:00 PM
  • Friday
    8:00 AM - 7:00 PM
Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?